Auswahl der wissenschaftlichen Literatur zum Thema „Utamaduni“

Geben Sie eine Quelle nach APA, MLA, Chicago, Harvard und anderen Zitierweisen an

Wählen Sie eine Art der Quelle aus:

Machen Sie sich mit den Listen der aktuellen Artikel, Bücher, Dissertationen, Berichten und anderer wissenschaftlichen Quellen zum Thema "Utamaduni" bekannt.

Neben jedem Werk im Literaturverzeichnis ist die Option "Zur Bibliographie hinzufügen" verfügbar. Nutzen Sie sie, wird Ihre bibliographische Angabe des gewählten Werkes nach der nötigen Zitierweise (APA, MLA, Harvard, Chicago, Vancouver usw.) automatisch gestaltet.

Sie können auch den vollen Text der wissenschaftlichen Publikation im PDF-Format herunterladen und eine Online-Annotation der Arbeit lesen, wenn die relevanten Parameter in den Metadaten verfügbar sind.

Zeitschriftenartikel zum Thema "Utamaduni"

1

Sululu, Simiyu Benson, Richard Makhanu Wafula und Joseph Nyehita Maitaria. „Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana“. East African Journal of Swahili Studies 3, Nr. 1 (02.08.2021): 91–99. http://dx.doi.org/10.37284/jammk.3.1.373.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Usomaji wa fasihi katika kipindi cha sasa unabainisha idadi kubwa ya waandishi kutoka jamii zisizo Waswahili ambao wameandika kazi katika tanzu mahsusi za fasihi simulizi ya Kiswahili. Waandishi hawa wameendelea kutumia maudhui, ploti na vipengele vingine vya utamaduni wa fasihi simulizi za jamii zao katika kubuni kazi zao za fasihi andishi ya Kiswahili. Vipengele vya fasihi simulizi za jamii za waandishi hawa, wasiokuwa Waswahili, vimeingizwa katika riwaya ya Kiswahili na kuwa sehemu ya riwaya hii. Makala hii imechunguza jinsi uingizaji wa vipengele hivi vya fasihi simulizi za watunzi wa riwaya ya Kiswahili, wasiokuwa Waswahili, unaifanya riwaya hii kuwa ya kimahuluti. Mahsusi, makala hii imedadavua mchango wa tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi katika umahuluti wa riwaya ya Kiswahili kupitia mfano wa riwaya ya Kufa Kuzikana (2003) iliyoandikwa na Ken Walibora. Tathmini hii imetumia Nadharia ya Umahuluti wa Utamaduni inayoshikilia kwamba panapotokea hali ya mtagusano baina ya tamaduni tofauti, matokeo yake si wingi-tamaduni bali ni mchanganyiko wa vipengele kutoka tamaduni hizi mbalimbali ambao ni bora na imara zaidi kuliko tamaduni asilia. Nadharia hii imetumiwa kufafanua jinsi umahuluti wa riwaya ya Kiswahili umechangiwa na uingizaji wa vipengele vya tanzu za kimaigizo za fasihi simulizi kutoka jamii za watunzi wake teule wasiokuwa Waswahili. Katika kufanya hivyo, makala hii imebainisha jinsi kuingizwa kwa vipengele hivi vya fasihi simulizi za jamii za waandishi teule katika riwaya ya Kiswahili kumeirutubisha riwaya hii kwa kuifanya kuwa changamano na nyumbufu kwa ambavyo inameza tanzu kutoka tamaduni tofauti na kujiimarisha kupitia kwazo bila kupoteza sura yake asilia.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
2

Wanyenya, Willy, Rocha Chimerah und Nancy Jumwa Ngowa. „Athari za Usasa kwenye Usimulizi wa Hadithi katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda“. East African Journal of Swahili Studies 2, Nr. 2 (08.09.2020): 116–27. http://dx.doi.org/10.37284/eajss.2.2.206.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Katika makala haya, watafiti anaeleza jinsi usimulizi wa hadithi umeathiriwa na usasa katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Anafanya hivyo kwa kulinganisha hali ilivyo sasa na jinsi ilivyokuwa kabla Wazungu hawajazuru barani Afrika. Mtafiti analinganisha miktadha ya utendaji wa hadithi na anatoa maelezo kuhusu mitindo mbalimbali ya utendaji. Anaeleza jinsi Waafrika walivyosimulia watoto wao hadithi kabla ya Wazungu kuja barani humu. Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni: kudhihirisha athari za usasa kwenye masimulizi ya kinathari. Pili, kueleza stadi zilizokuwa zikitumiwa na Waafrika katika usimulizi wa hadithi. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani halafu akaanza kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Kabla hajafanya hivyo, mtafiti alijitambulisha kwa wahojiwa wake na kuwaambia sababu za utafiti wake. Alifanya hivyo ili kuwaondolea wasiwasi. Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usimulizi wa hadithi umefifia sana katika jamii ya Wamasaaba kutokana na usasa. Sababu ambazo zimepelekea usimulizi wa hadithi kufifia jamii hii pia zimeelezwa. Miongoni mwa sababu hizo ni: ulevi ambao hufanya watu kurejea nyumbani wakiwa wamelewa na kushindwa kusimulia watoto wao hadithi. Sababu nyingine ni wazazi kuthamini elimu ya kisasa na kuacha utamaduni wao wa kulea watoto ili baadaye wawe wake na waume wazuri. Wazazi kuhamasisha watoto wao wasome vitabu badala ya kuwasimulia hadithi. Nne, wazazi kuwa na lengo la kuelimisha watoto wao ili baadaye wapate kazi za afisi. Tano, jambo la kuwepo na utandawazi ambalo limepelekea watu kujumuika na kuiga tamaduni za kigeni. Upeo wa utafiti huu ulihusika na mabadiliko kwenye usimulizi wa hadithi na sababu ambazo zimepelekea utamaduni wa kusimulia hadithi kufifia katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Mtafiti alitumia mbinu ya bahati nasibu kuteua sampuli za wahojiwa.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
3

Migodela, Willy. „Dhamira za Maandishi ya Kuta za Vyooni Jijini Dar es Salaam“. Mkwawa Journal of Education and Development 1, Nr. 1 (01.12.2017): 17–27. http://dx.doi.org/10.37759/mjed.2017.1.1.2.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Makala haya yanahusu dhamira za maandishi, hususani ya vyooni Jijini Dar es Salaam. Lengo ni kuangalia dhamira za maandishi hayo na nafasi yake kwa jamii. Katika uchambuzi tumetathmini ubunifu unaojitokeza katika maandishi hayo. Aidha, kwa kutumia mbinu za utafiti maktabani kama vile uchambuzi matini na mbinu za uwandani, tulipata data muafaka kuhusu suala la kiutafiti lililoshughulikiwa katika makala haya. Pia, tumedurusu maandiko mbalimbali yanayozungumzia dhamira katika maandishi yaliyoandikwa sehemu mbalimbali na namna lugha ilivyotumika kutoa mawasiliano. Aidha, tumetumia nadharia ya Elimu-mitindo ambayo ndiyo inayoongoza uchambuzi na mjadala katika makala haya. Hali kadhalika, kutokana na utafiti huu, imebainika kuwa dhamira zilizojitokeza zaidi ni zile zinazohusu maradhi, maarifa, maadili na dini. Ilibainika pia kuwa dhamira hizi zinaakisi muundo na mfumo wa maisha ya jamii husika. Kutokana na matokeo haya, imehitimishwa kuwa ubunifu uliopo kwenye maandiko ya vyooni unasawiri hali mbalimbali katika jamii kama vile mtazamo wa wanajamii kuhusu maana na umuhimu wa elimu, dini, maadili na utamaduni kwa ujumla. Hatimaye, katika makala haya tutaona jinsi lugha safihi (matumizi ya lugha yasiyo na adabu) inavyojitokeza katika maandishi ya vyooni.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
4

Prof. Wendo Nabea, Harrison Onyango Ogutu; Dr Sheila Wandera;. „Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi“. Editon Consortium Journal of Kiswahili 2, Nr. 1 (30.06.2020): 76–88. http://dx.doi.org/10.51317/ecjkisw.v2i1.130.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Watu wenye uwezo na mamlaka wanatumia madaraka yao kuwatawala wengine kwa vishawishi anuwai. Asasi za kijamii kama vile ndoa, shule, vyuo, utamaduni na malezi zinaendelea kushuhudia utawala wa wenye uwezo juu ya wasio na uwezo. Licha ya ubayana wa hali hii katika jamii, watafiti na wahakiki wa tanzu za fasihi andishi hususan riwaya hawajaonyesha namna hejemonia inajitokeza katika asasi za kijamii. Ingawa wahakiki wengi wa riwaya wameweza kuangazia masuala ya kila nui kuhusu asasi za kijamii, suala la hejemonia katika taasisi hizo lilihitaji kumulikwa. Hivyo, utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ujitokezaji wa hejemonia katika safu ya hejemonia ya jamii kwa mujibu wa riwaya za Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya hejemonia ilioasisiwa na Antonio Gramsci katika makala aliyoyaandika akiwa gerezani kati ya mwaka wa 1923 na 1936. Nadharia hii inaelezea udumishaji wa uwezo na mamlaka ya tabaka moja kuu juu ya tabaka dogo kwa kutumia mikakati anuwai. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani ambako utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kithamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Matokeo ya utafiti huu yatawafaa wahakiki na watafiti wa lugha na fasihi huku yakiweka wazi uwepo wa hejemonia katika asasi za jamii.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
5

Mwanakombo Mohamed; Mosol Kandagor, Jane Jepkoech Singoei;. „Jinsi Vipengele vya Kitamaduni katika Matini Teule ya Kiswahili na Kikalenjin Vilivyochangia Mtafsiri Kuiandika Upya Bukuit Ne Tilil.“ Editon Consortium Journal of Kiswahili 2, Nr. 1 (30.09.2020): 110–24. http://dx.doi.org/10.51317/ecjkisw.v2i1.155.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya Kiswahili na Kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu, ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubaini kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri. Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa: utamaduni wa Waswahili na wa Wakalenjin ni tofauti na hii ilipelekea uandishi upya ufanywe katika tafsiri. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Sera za elimu kuhusu lugha za kienyeji zinafaa kutilia maanani tafsiri ya matini za kufundishia.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
6

Ogutu, Wanyama. „Halafu ya Sanaa za Ubunifu wa Kiafrika: Mtanziko Rejeleshi wa Tawala za Kiafrika“. East African Journal of Swahili Studies 3, Nr. 1 (01.06.2021): 24–29. http://dx.doi.org/10.37284/jammk.3.1.334.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Mwonekano wa aliyekuwa rais wa Zaire; Kukugbedu Zambanga Seseseko Mobuto kwenye Umoja wa Mataifa huko New York ulirejesha maisha ya baadaye ya ubunifu wa Kiafrika. Ufanisi wa marejeo ya ubunifu wa Kiafrika umeleta sheria, kuwapo kwa sheria za kitaifa na mikataba ya maafikiano na ujima katika baraza la mataifa la makavazi katika mataifa ya Afrika. Karatasi hii ni makala ya maoni kwa (Africa Union-AU) Jumuia ya Afrika mwaka 2021 Mwaka wa Sanaa ya Uchoraji, Turathi na Utamaduni. Dhamira ya mtafiti ni kutatua mtanziko wa urejeo wa ubunifu wa sanaa ya Kiafrika katika taifa la Afrika. Lengo limebainisha baadhi ya vikwazo vinavyofanya urejeshi wa ubunifu wa sanaa ya Kiafrika kuwa mgumu hasa katika nchi yake ya asili. Karatasi hii imechambua sauti ya kitaalam katika marejeleo ya fasihi, makala na vitabu vya kisasa kuhusu Sanaa ya uchoraji ya Afrika. Imeteua bila taratibu maalum, sampuli kadhaa za utawala wa zamani wa Uropa Afrika kama vile Uingereza, Ufaransa, na Italia miongoni mwa mengine katika mijadala yake kama mifano. Kuafiki ajenda ya Jumuia ya Afrika mwaka wa 2063, karatasi imeamua kuwa kuwapo kwa mijadala ya kina kuhusu kurejea katika makongamano ya kimataifa yaliyoandaliwa na Jumuia ya Afrika. Kurejeshwa huku kutawapa wataalamu wa Kiafrika jukwaa la kuzidisha utafiti wa jambo la urejesho wa mali ya kitamaduni kwa taifa asilia, ili kuleta suluhu mwafaka na halisi. Mwisho, ina ombi kwa wakuu wa mataifa na nchi za Afrika walio mamlakani kuwa mstari wa mbele katika kunadi habari zaidi kuhusu turathi za kitamaduni duniani. Mataifa ya Afrika yalete kazi zake asilia, halisi na bora zaidi za sanaa ya uchoraji, minara na sanamu, vifaa vya dini, alama na ishara za kitaifa, mabaki ya mababu na kazi za sanaa bunifu zilizovurugika.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
7

Oketch, Samson Ezekiel, Beverlyne Asiko Ambuyo und Rosemary Makokha. „Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili“. East African Journal of Swahili Studies 2, Nr. 1 (10.04.2020): 8–18. http://dx.doi.org/10.37284/eajss.2.1.135.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jamii. Tafiti nyingi zilizofanywa zinahusu vipengele vya fasihi kama vile maudhui, matumizi ya lugha, wahusika na mandhari katika fasihi. Katika tafiti hizo, watafiti hawajaonyesha mifumo jamii inayojitokeza kutokana na vipengele hivi. Utafiti huu umezama na kiutathimini mifumo hii kupitia kwa tamthilia teule za Kiswahili ambazo ni: tamthilia ya Pango (2003) kilichoandikwa na Wamitila, Kifo Kisimani (2008) kilichoandikwa na Kithaka Wa Mberia na Mstahiki Meya (2009) kilichoandikwa na Timothy Arege. Mifumo iliyotafitiwa katika utafiti huu ni: mfumo wa utawala na siasa, wa uchumi katika jamii, wa utamaduni, wa imani na dini, ule wa tabaka za jamii na ule wa elimu ya jamii. Utafiti huu umeongozwa na madhumuni mahsusi yafutayo: kujadili maudhui yanayodhihirisha mifumo ya jamii katika tamthilia teule; kuchanganua mitindo ya lugha inavyodhihirisha mifumo ya kijamii kutoka tamthilia teule; na kuchunguza wahusika katika uhusika wao kwenye mandhari maalumu wanavyojenga ploti inayochangia kuweka wazi mifumo ya kijamii kutoka tamthilia teule. Kiunzi cha nadharia ya uchunguzi kimejengwa na nadharia za uhalisia na nadharia ya umtindo. Mihimili ya nadharia ya uhalisia ikiwemo masuala ya utawala na uongozi, yale ya vijana, udhanifu, ukosefu wa ajira na masuala ya jinsia imebainishwa kadri ilivyojitokeza kupitia tamthilia teule. Mbali na nadharia za uhalisia na umtindo nadharia ya ukoloni mamboleo imetumika kuelezea hali katika tamthilia hasa utambuzi wa mifumo jamii inayotokana na matokeo ya baada ya uhuru. Utafiti umeongozwa na tamthilia 26 zilizoandikwa nchini Kenya na Tanzania tangu mwaka wa 2000. Tamthilia 26 zilizotumika ni zile zilizoandikwa na wazawa asilia wa Afrika Mashariki na kati kufikia mwaka wa 2014. Asilimia kumi ya idadi hiyo ilipeana sampuli ya mbili nukta sita (2.6) ambacho ni kifani tosha cha tamthilia tatu. Utafiti huu umejikita Kenya na Tanzania kwa kigezo kuwa mbali na Kiswahili kuchimbukia na kuenea zaidi katika janibu hizi, imebainika pia kuwa sera na sheria za kikatiba za nchi hizi zimekipa Kiswahili kipao mbele. Orodha ya uchuzaji imetumika kukusanya data. Uchanganuzi wa data ulitumia yaliyomo. Utafiti huu unatarajiwa kuibua mawazo mapya kuhusu mifumo ya kijamii inayotokana na fasihi na hivyo kuchangia katika ukuaji wa elimu.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
8

Wesonga, Esther Lucy, Beverlyne Asiko Ambuyo und Rocha Chimerah. „Nafasi ya Fasihi Katika Kuwasilisha Masuala ya Mazingira Kupitia Riwaya Teule Tikitimaji (2013) na Msimu wa Vipepeo (2006) za K. W. Wamitila“. East African Journal of Swahili Studies 2, Nr. 2 (11.08.2020): 54–64. http://dx.doi.org/10.37284/eajss.2.2.192.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Suala la mabadiliko ya hali ya anga ni janga linaloendelea kukumba ulimwengu kwa jumla. Kutokuwepo kwa usawazishaji wa ekolojia ni jambo ambalo linawatia shaka adinasi wengi. Fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kuwasilisha hali halisi ya maisha ya binadamu. Utafiti huu unachambua nafasi ya fasihi katika kuwasilisha masuala ya mazingira kupitia riwaya mbili teule za Wamitila, Tikitimaji (2013) na Msimu Wa Vipepeo (2006). Mwandishi huyu ameonyesha ari katika uwanja wa fasihi mazingira, kwenye makala yake ya “Place and placelessness in Kiswahili literature: The role of setting in Kiswahili creative writing” anasema kuwa mandhari huchukua nafasi katika kuwasilisha masuala ya mazingira. Kazi hii ilichunguza namna mwandishi alivyotumia fasihi kuwasilisha masuala ya mazingira katika riwaya zake za hivi karibuni. Ingawa kwa miaka mingi, masuala ya mazingira yamehusishwa na sayansi haswa katika kutoa takwimu kamilifu kuhusiana na masuala ya mazingira, fasihi inaendelea kuchukua dhima mpya katika jamii inayozidi kukua kiteknolojia. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni yafuatayo: kubainisha jinsi mwandishi wa riwaya ya Tikitimaji alivyotumia wahusika ili kuwasilisha maudhui ya mazingira. kueleza mitindo ya lugha iliyotumiwa kuwasilisha masuala ya mazingira na tatu, kutathimini iwapo mwandishi amefaulu kuwasilisha maudhui ya mazingira riwayani. Utafiti huu ulitumia kiunzi cha nadharia kutoka kwa nadharia ya fasihi mazingira na nadharia ya uhalisia. Mihimili zitakazotumiwa kutoka nadharia ya uhalisia ni: kazi ya fasihi imejitosheleza, kazi ya msanii inapaswa kuwasilisha ukweli, mtunzi anaangalia matatizo na kuchunguza chanzo chake na mwisho wahusika ni vielelezo yakini vya binadamu wa kawaida kwa vile wao hutumia lugha ya kawaida wanayoitumia humwezesha mwanadamu kujifafanulia uwezo wake wa kutenda mambo. Mihimili ya fasihi mazingira iliyotumika ni: kuangalia dhana za ekolojia katika kazi za fasihi, mitindo na uwezo wa lugha na jinsi mitindo hiyo huathiri namna binadamu anavyotagusana na mazingira na mwisho binadamu hawezi ishi bila ekolojia lakini ekolojia huweza kuishi bila binadamu. Data ilipangwa kwenye makundi na kuchanganuliwa kwa kuzingatia madhumuni ya utafiti na mihimili ya kiunzi cha nadharia. Data iliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu umelenga kuhamasisha wasomi na waandishi wa fasihi wajikite zaidi kulenga masuala ya mazingira ambayo ndicho kitovu cha maisha ya binadamu. Utafiti ulibaini kuwa fasihi ni nyenzo mwafaka ya kuwasilisha masuala ya mazingira kupitia vipengele vyake. Kwani huingiliana sana na utamaduni wa jamii.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
9

Syamsudin, Kinkin. „MANHAJ IBNU ABÎ HÂTIM DALAM KITAB AL-JARH WA AL-TA’DÎL“. Diroyah : Jurnal Studi Ilmu Hadis 2, Nr. 1 (22.05.2018): 1–14. http://dx.doi.org/10.15575/diroyah.v2i1.2491.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
-newline"> Artikel ini membahas mengenai manhaj Ibnu Abî Hâtim dalam penulisan Kitab Al-Jarh wa al-Ta’dil.Pada masanya kitab ini menjadi salah satu rujukan utama untuk mengetahui riwayat hidup dan kualitaspara rawi. Dengan mencantumkan 18.040 rawi di dalamnya, Ibnu Abî Hâtim telah ikut berkontribusidalam menyediakan data tentang para priwayat hadis. Dari kitab tersebut, salah satunya bisa diketahuikomentar-komentar para kritikus hadis tentang keadaan setiap perawi, apakah diterima (maqbul) atauditolak (mardud) sehingga nantinya bisa ditentukan status dan derajat hadis yang diriwayatkan olehperawi tersebut. Dengan menggunakan metode studi pustaka (Library Research) dan melalui pendekatananalisis isi (content analysis), akhirnya bisa diketahui bahwa penilaian Ibnu Abî Hâtim tehadap para rawitidak terlepas dari subjektivitas penulisnya sendiri dan cenderung tetap menyandarkan informasi utamadari para kritikus generasi sebelumnya. Dan setelah dikomparasikan dengan kitab kritikus lainnya yangsemisal, akhirnya idealisme Ibnu Abî Hâtim dalam kitab tersebut tidak tersinkronkan antara konsep danrealistasnya.
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
10

Arvenia, Rica, Muhammad Fedryansyah und Muhamad Fadhil Nurdin. „Giddens dan Kapitalisme: Etika Kerja Buruh Perkebunan Karet di Sumatera Selatan“. Jurnal Pemikiran Sosiologi 5, Nr. 2 (01.04.2019): 108. http://dx.doi.org/10.22146/jps.v5i2.44637.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
Industri karet berkaitan pada kondisi buruh dan penguasaan wilayah, serta masuknya sistemkapitalisme dalam sektor perkebunan karet. Modernitas yang terjadi menjadi beban bagi buruh kerjaperkebunan karet karena sistem-sistem modern telah masuk dan dimiliki oleh sistem kapitalisme,sehingga menjadi dampak buruk bagi buruh, kesejahteraan merupakan bagian terpenting dalamsektor industri maupun perkebunan. Artikel ini berfokus pada masalah kapitalisme dan etika kerjayang ada pada perkebunan karet di Sumatera Selatan, dengan menggunakan pendekatan kualitatifdan analisis deskriptif.Teknik pengumpulan data berupa studi literatur, jurnal, observasi, sertawawancara mendalam pada pemilik kebun karet dan buruh perkebunan karet. Hasil penelitianmenunjukkan bahwa: (1) terjadinya sistem kapitalisme pada perkebunan karet yang diakibatkanoleh ketikstabilan harga. (2) etika kerja pada perkebunan karet direproduksi oleh perorangan, (3)terjadinya modernitas memberikan dampak pada harapan buruh perkebunan dan menjadi bebanbagi pemilik untuk mensejahterahkan buruh. Dalam teori strukturisasi yang dikemukakan olehGiddens ialah bahwa perubahan struktur dipengaruhi oleh agen dan struktur sehingga kunci utamadari kesejahteraan ada pada sistem, sistem yang tidak baik dapat membawa dampak yang buruk
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen

Dissertationen zum Thema "Utamaduni"

1

Kariuki, Lydiah Wanjiru. „An exploration of alcohol abuse as a risk factor for Intimate Partner Violence in Kibera, Kenya“. Diss., 2021. http://hdl.handle.net/10500/27552.

Der volle Inhalt der Quelle
Annotation:
The purpose of this study was to explore the influence of alcohol abuse on intimate partner violence (IPV) committed in Kibera, Kenya. The study is premised on the high prevalence of IPV and alcohol abuse in Kenya, especially among informal settlement dwellers. Kenya is geographically located in Eastern Africa. Kibera is an informal settlement in the country’s capital city, Nairobi, and is plagued by extreme poverty, unemployment and crime. A qualitative approach was implemented and a case study research design employed. Non-probability sampling, using purposive and snowball techniques, was used to select research participants. A total of 32 female victims of IPV made up the sample used in the study. Although the study did not intend to exclude males from the sample, no male victims of IPV could be located. Semi-structured interviews were held individually with each participant. Ethical considerations were actively applied throughout the duration of the study. The raw data collected were thematically analysed. The findings of the study revealed that most of the participants were under 40 years old, married, and had at least one child. Their educational levels were limited, and their occupations as well as their partners’ occupations generated low incomes. Physical and psychological abuse were cited as the most common types of abuse. However, sexual abuse was still prevalent and in some cases was extended to the children. The physical and psychological impacts were identified as the most prevalent effects of IPV. The effects on the children and family were also explored. The study found a strong link between alcohol use and IPV. However, alcohol use and/or abuse could not be identified as the only causal factor of IPV. Interestingly, the participants’ experiences highlighted the patriarchal and cultural milieu significant to Kibera. It was found that the patriarchal nature maintained in Kibera is one of the factors contributing to IPV and its perpetuation.
Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari za pombe kwa dhuluma zinazosababishwa na mpenzi unayeshiriki naye ngono (IPV) katika eneo la Kibera nchini Kenya. Utafiti huu unatokana na kiwango cha juu cha hali ya IPV na unywaji wa pombe kupindukia nchini Kenya, hasa kwa wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda. Kenya hupatikana katika eneo la kijiografia la Afrika Mashariki. Kibera ni mtaa wa mabanda ambao unapatikana katika mji mkuu wa Nairobi. Kibera inakabiliwa na umasikini uliokithiri, ukosefu wa ajira na uhalifu. Mbinu ya kutathmini ubora ilitumika, na uchunguzi kifani ulitumika. Sampuli isiyokuwa na welekeo wa uwezekano ilitumika, kwa kutumia mbinu za kimakusudi, na kwa kuongeza mambo utafiti unapoendelea wakati wa kuchagua watu wa kushiriki kwenye utafiti. Jumla ya waathiriwa wa IPV 32 wa kike walitumika kama sampuli katika utafiti huu. Ijapokuwa utafiti haukuwa na lengo la kutowashirikisha wanaume, hakuna muathiriwa wa IPV wa kiume alipatikana. Maswali yaliyokuwa na utaratibu maalum yalitumika kwa kila mshiriki. Maadili yalizingatiwa mno wakati wa mchakato mzima wa utafiti. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia mada. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa wengi wa washiriki waliokuwa na umri usiozidi miaka 40, walikuwa wameolewa na angalau mtoto mmoja. Hawakuwa wamesoma mno, na wao pamoja na wapenzi wao walikuwa na ajira zenye ujira duni. Kupigwa na kuteswa kisaikolojia ni dhuluma zilizojitokeza mno. Hata hivyo, unyanyasaji wa kimapenzi bado ulishuhudiwa na hata wakati mwingine ulifanyiwa watoto. Madhara kwa mwili na ya kisaikolojia yalijitokeza kama athari kuu za IPV. Athari kwa watoto na kwa familia pia zilichunguzwa. Utafiti huu ulionyesha kuwa kuna uhusiano mkuu kati ya matumizi ya pombe kupindukia na IPV. Hata hivyo, matumizi ya pombe/au kulewa kupindukia siyo tu mambo yanayosababisha IPV. Cha kushangaza, hali zilizoelezwa na washiriki zilionyesha umuhimu wa mfumo dume kwa utamaduni wa watu wa Kibera. Iligunduliwa kuwa mfumo wa udume unaoendelea katika eneo la kibera, ni mojawapo wa mambo yanayochangia IPV na kuendelezwa kwake Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari za pombe kwa dhuluma zinazosababishwa na mpenzi unayeshiriki naye ngono (IPV) katika eneo la Kibera nchini Kenya. Utafiti huu unatokana na kiwango cha juu cha hali ya IPV na unywaji wa pombe kupindukia nchini Kenya, hasa kwa wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda. Kenya hupatikana katika eneo la kijiografia la Afrika Mashariki. Kibera ni mtaa wa mabanda ambao unapatikana katika mji mkuu wa Nairobi. Kibera inakabiliwa na umasikini uliokithiri, ukosefu wa ajira na uhalifu. Mbinu ya kutathmini ubora ilitumika, na uchunguzi kifani ulitumika. Sampuli isiyokuwa na welekeo wa uwezekano ilitumika, kwa kutumia mbinu za kimakusudi, na kwa kuongeza mambo utafiti unapoendelea wakati wa kuchagua watu wa kushiriki kwenye utafiti. Jumla ya waathiriwa wa IPV 32 wa kike walitumika kama sampuli katika utafiti huu. Ijapokuwa utafiti haukuwa na lengo la kutowashirikisha wanaume, hakuna muathiriwa wa IPV wa kiume alipatikana. Maswali yaliyokuwa na utaratibu maalum yalitumika kwa kila mshiriki. Maadili yalizingatiwa mno wakati wa mchakato mzima wa utafiti. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia mada. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa wengi wa washiriki waliokuwa na umri usiozidi miaka 40, walikuwa wameolewa na angalau mtoto mmoja. Hawakuwa wamesoma mno, na wao pamoja na wapenzi wao walikuwa na ajira zenye ujira duni. Kupigwa na kuteswa kisaikolojia ni dhuluma zilizojitokeza mno. Hata hivyo, unyanyasaji wa kimapenzi bado ulishuhudiwa na hata wakati mwingine ulifanyiwa watoto. Madhara kwa mwili na ya kisaikolojia yalijitokeza kama athari kuu za IPV. Athari kwa watoto na kwa familia pia zilichunguzwa. Utafiti huu ulionyesha kuwa kuna uhusiano mkuu kati ya matumizi ya pombe kupindukia na IPV. Hata hivyo, matumizi ya pombe/au kulewa kupindukia siyo tu mambo yanayosababisha IPV. Cha kushangaza, hali zilizoelezwa na washiriki zilionyesha umuhimu wa mfumo dume kwa utamaduni wa watu wa Kibera. Iligunduliwa kuwa mfumo wa udume unaoendelea katika eneo la kibera, ni mojawapo wa mambo yanayochangia IPV na kuendelezwa kwake Utafiti huu utakuwa na manufaa kwa waathiriwa wa IPV, jamii wanazotoka na watungaji wa sheria za kitaifa bila kusahau jamii ya watafiti wa kisayansi.
Maikemisetso a thutopatlisiso eno e ne e le go tlhotlhomisa tshusumetso ya tiriso e e botlhaswa ya nnotagi mo tirisodikgokeng ya balekane ba baratani (IPV) e e diragalang kwa Kibera, Kenya. Thutopatlisiso e theilwe mo tiragalong e e kwa godimo ya IPV le tiriso e e botlhaswa ya nnotagi kwa Kenya, bogolo segolo magareng ga banni ba mafelo a baipei. Kenya e fitlhelwa kwa Botlhaba jwa Aforika. Kibera ke lefelo la baipei mo motsemogolong wa naga, Nairobi, mme e aparetswe ke lehuma, botlhokatiro le bosenyi jo bo boitshegang. Go dirisitswe molebo o o lebelelang mabaka mme ga dirisiwa thadiso ya thutopatlisiso e e lebelelang kgetse. Go dirisitswe mokgwa wa go tlhopha sampole moo baagi ba se nang tšhono e e tshwanang ya go nna le seabe le dithekeniki tsa go tlhopha sampole go ya ka maitlhomo le go letla banni-le-seabe ba pele go ngokela ba bangwe go tlhopha banni-le-seabe ba patlisiso. Palogotlhe ya batswasetlhabelo ba basadi ba IPV ba le 32 e nnile sampole e e dirisitsweng mo thutopatlisisong. Le fa thutopatlisiso e ne e sa ikaelela go se akaretse banna mo sampoleng, go ne go se na batswasetlhabelo bape ba IPV ba banna ba ba tlhageletseng. Go nnile le dipotsolotso tse di batlileng go rulagana tse di tshwerweng le monni-le-seabe mongwe le mongwe ka sebele. Go dirisitswe ntlha ya maitsholo a a siameng ka botlhaga mo tsamaong ya thutopatlisiso yotlhe. Data e e kokoantsweng e ne ya lokololwa go ya ka meono. Diphitlhelelo tsa thutopatlisiso di senotse gore bontsi jwa banni-le-seabe ba ne ba le dingwaga tse di kwa tlase ga 40, ba nyetswe mme ba na le bonnye ngwana a le mongwe. Seelo sa bona sa thuto se ne se lekanyeditswe mme ditiro tsa bona gammogo le tsa balekane ba bona di ne di tsenya letseno le le kwa tlase. Tshotlakako ya mo mmeleng le ya maikutlo di tlhagisitswe jaaka mefuta e e tlwaelegileng thata ya tshotlakako. Le gale, tshotlakako ya thobalano e ne e ntse e le teng mme mo mabakeng mangwe e ne e fetela le mo baneng. Ditlamorago tsa mo mmeleng le mo tlhaloganyong di supilwe jaaka ditlamorago tse di bonalang thata tsa IPV. Go lebeletswe le ditlamorago mo baneng le mo lelapeng. Thutopatlisiso e fitlhetse go na le kgolagano e e maatla magareng ga tiriso ya nnotagi le IPV. Le gale, tiriso le/gongwe tiriso e e botlhaswa ya nnotagi ga e a supiwa e le yona fela ntlha e e bakang xi IPV. Se se kgatlhisang ke gore maitemogelo a banni-le-seabe a senotse ka moo tsamaiso e e letlang banna go laola basadi le setso di laolang basadi ka gona mo loagong e leng se se maleba tota kwa Kiberia. Go fitlhetswe gore tsamaiso ya setšhaba e e letlang banna go laola basadi e e tswelediwang kwa Kiberia ke nngwe ya dintlha tse di tshwaelang le go etegetsa IPV. Thutopatlisiso e lebeletse go ungwela batswasetlhabelo ba IPV, baagi ba selegae le lekgotlataolo la bosetšhaba, gammogo le dipatlisiso tsa saense.
Criminology and Security Science
M.A. (Criminology)
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen

Bücher zum Thema "Utamaduni"

1

Mbaabu, Ireri. Utamaduni wa Waswahili. Nairobi, Kenya: Kenya Pub. & Book Marketing Co., 1985.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
2

Utamaduni wa Mzanzibari. Zanzibari: Baraza la Kiswahili la Zanzibar, 2008.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
3

Historia ya Kilwa na utamaduni wa wakazi. Dar es Salaam: Tanzania Pub. House, 2003.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
4

Hagamu, Emil C. N. Dumisha uhai: Mapambano dhidi ya utamaduni wa kifo. Dar es Salaam: Pro-Life (HLI) Tanzania, 2004.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
5

Geiger, Susan. Wanawake wa TANU: Jinsia na utamaduni katika kujenga uzalendo Tanganyika, 1955-1965. Dar es Salaam: TGNP, 2005.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
6

Fasihi simulizi na utamaduni: Kitabu cha walimu na wanafunzi, (shule na vyuo). Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation, 2008.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
7

Elieshi, Lema, und Tanzania Gender Networking Programme, Hrsg. Wanawake wa TANU: Jinsia na utamaduni katika kujenga uzalendo Tanganyika, 1955-1965. Dar es Salaam: TGNP, 2005.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
8

Makumbusho ya Dar es Salaam: Ijue historia yako : urithi wa utamaduni : Kilwa Kisiwani. [Dar es Salaam]: Charles Computer Graphics Designer, 2004.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
9

Moshi, Lioba J. Kiswahili language and culture: A textbook for the teaching of Kiswahili with video = Kiswahili : lugha na utamaduni : kitabu cha mwanafunzi wa Kiswahilli kwa video. Kensington, Md: Dunwoody Press, 1998.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
10

K, Mlacha S. A., Hurskainen Arvi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. und Helsingin yliopisto. Aasian ja Afrikan kielten ja kulttuurien laitos., Hrsg. Lugha, utamaduni na fasihi simulizi ya Kiswahili: FASIHI YA KISWAHILI. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1995.

Den vollen Inhalt der Quelle finden
APA, Harvard, Vancouver, ISO und andere Zitierweisen
Wir bieten Rabatte auf alle Premium-Pläne für Autoren, deren Werke in thematische Literatursammlungen aufgenommen wurden. Kontaktieren Sie uns, um einen einzigartigen Promo-Code zu erhalten!

Zur Bibliographie